Magufuli kufanya ziara siku tatu Dar

22Feb 2021
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM
Nipashe
Magufuli kufanya ziara siku tatu Dar

Rais Dk. John Magufuli anatarajiwa kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu Jijini Dar es Salaam, ambapo katika ziara hiyo atazindua miradi mbalimbali ya maendeleo.

Rais Dk. John Magufuli.

Akizungumza kuhusu ziara hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakar Kunenge amesema ziara hiyo itaanza Jumatano ya Februaryi 24,2021 ambapo atazindua Daraja la Juu Ubungo (Ubungo Interchange) majira ya saa 03:30 asubuhi na mara baada ya hapo ataelekea Mbezi kwa ajili ya uzinduzi wa Kituo ca Mabasi yaendayo mikoani na nje ya nchi cha Mbezi Luis majira ya saa 05:30 asubuhi.

RC Kunenge, amesema siku ya Alhamis Februari 25,2021 Rais Dk. Magufuli anatarajiwa kuweka jiwe la msingi la Ujenzi wa Soko la kisasa Kisutu majira ya saa 03:30 asubuhi na baada ya hapo atafanya shughuli ya uzinduzi wa jengo la Jitegemee House ambapo kuna Studio za Channel ten na Uhuru Fm.

Amesema siku ya Ijumaa ya Februari 26,2021 Rais Magufuli atafanya shughuli ya uzinduzi wa Majengo ya Chuo cha Polisi na Kiwanda cha kutengeneza sare za Polisi tukio litakalofanyika Saa 03:30 asubuhi.

Habari Kubwa