Mahakama yakataa ombi la DC Odunga kutaliki

23Aug 2019
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Mahakama yakataa ombi la DC Odunga kutaliki
  • Yamtaka kutoa Sh250,000 kila mwezi kwa ajili ya matunzo ya mtoto

 Mahakama ya Mwanzo ya Ukonga, Dar es Salaam imekataa ombi la Mkuu wa Wilaya ya Chemba mkoani Dodoma, Simon Odunga kumtaliki Ruth Osoro.

Mkuu wa Wilaya ya Chemba mkoani Dodoma, Simon Odunga kushoto akiwa na mke wake wa nje ndoa Ratifa vicent katika mahakama ya ukonga.

Hakimu Elia Mrema ametoa hukumu hiyo leo Ijumaa Agosti 23,2019  baada ya kusikiliza ushahidi uliotolewa na mashahidi wa pande zote.

Mbali na kukataa ombi la talaka, imemuamuru Odunga kutoa Sh250,000 za matunzo kila mwezi kwa mtoto wao huyo mwenye umri wa miaka minne kuanza sasa hadi atakapofikisha umri wa miaka 18 pamoja na kugharamia matibabu na masomo ya mwanaye.

Hakimu Mrema amesema kulingana na cheti cha ndoa iliyofungwa bomani kati ya Odunga na Ruth inaonyesha mkuu huyo wa wilaya hajawahi kuoa wala mdaiwa hajawahi kuolewa.

Licha ya malalamiko hayo Ruth aliomba Mahakama isivunje ndoa yake kwa kuwa bado anampenda mume wake huku Odunga akitaka ndoa ivunjwe na apewe ridhaa ya kumlea mtoto huyo.

Lakini kabla ya kuhitimisha cheti hicho cha ndoa, Mahakama ilikilinganisha na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na Odunga ambao haukuwa na uwazi kuwa wakati anamuoa Ruth mwaka 2010, mwanamke huyo alikuwa akitambua kuwa  anaishi na mwanamke mwingine na akaridhia.

Imeandikwa na Rahma Kisilwa, TUDARCo

 

 

 

 

 

 

Habari Kubwa