Mahakama yataka makosa uhujumu uchumi kuendelea kutokuwa na dhamana

05Aug 2020
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM
Nipashe
Mahakama yataka makosa uhujumu uchumi kuendelea kutokuwa na dhamana

Mahakama ya Rufaa Tanzania imetengua uamuzi wa awali wa Mahakama Kuu na kusema makosa yaliyochini ya kifungu cha 148 (5) ya CPA mfano makosa ya uhujumu uchumi na utakatishaji fedha yaendelee kuwa hayana dhamana.

Wakili Mkuu wa Serikali Gabriel Malata, (kushoto) akiwa ndani ya ukumbi wa Mahakama ya Rufani akisubiri kusomwa kwa uamuzi katika shauri linalohusu kufutwa kwa kifungu cha dhamana kwa makosa makubwa ya jinai unaotarajiwa kusomwa leo Mahakamani hapo.

Rufaa hiyo inapinga uamuzi wa Mahakama kwenye Shauri la Madai Namba 08 la 2019 ambapo Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala ya Dar es Salaam ilimpatia ushindi Bw. Sanga mnamo Tarehe 18 Mei 2020.

Mahakama Kuu iliiagiza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kurekebisha kifungu hicho ndani ya miezi 18 kutoka siku ya kutolewa kwa hukumu huku ikiionya Jamhuri kuwa kushindwa kufanya hivyo kutasababishwa kufutwa.

 

Habari Kubwa