Mahakimu watakiwa kutenda haki usikilizwaji mashauri 

07Aug 2020
Marco Maduhu
Shinyanga.
Nipashe
Mahakimu watakiwa kutenda haki usikilizwaji mashauri 

Jaji Mkuu wa Tanzania Prof Ibrahimu Juma, amewataka Mahakimu wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga, kutenda haki kwa wananchi wote bila ya ubaguzi wa kujali hali zao wakati wa usikilizaji wa mashauri mahakamani.

Jaji mkuu wa Tanzania Prof Ibrahimu Juma, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Jengo la Mahakama kuu ya Kanda ya Shinyanga, na kuwataka Mahakimu kutenda haki wakati wa usikilizaji wa mashauri.

Amebainisha hayo leo wakati akizundua  rasmi Jengo la Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga, ambalo lilijengwa mwaka 2006 na kukamilika mwaka 2015 kwa gharama ya Shilingi bilioni 4.

Amesema jengo hilo limejengwa kwa madhumuni ya kutoa huduma kwa wananchi wote bila ya kujali hali zao, na kusiwepo na ubaguzi wakati wa usikilizaji wa mashauri, pamoja na uhairishaji wa mashauri hayo bila ya sababu za msingi.

Jaji mstaafu wa Tanzania Othman Chande, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Jengo la Mahakama kuu ya Kanda ya Shinyanga.

“Jengo hili la Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga limejengwa kwa ajili ya kusogeza huduma kuwa karibu na wananchi, na mahakama siku zote hua ni mali ya wananchi, hivyo naomba haki itendeke kwa wote wakati wa usikilizaji wa mashauri bila ya kujali hali zao,” amesema Prof Juma.

Naye Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Othmani Chande, amesema jengo hilo liwe msaada kwa wananchi kusikilizwa mashauri yao ya rufaa kwa wakati, na kusitokee changamoto tena ya kuchelewa kusikilizwa, ili kuondoa utofauti wa zamani na kuonekana faida ya kujengwa Mahakama hiyo Kuu ya Rufaa Kanda ya Shinyanga.

Kwa upande wake Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Shinyanga, Gerson Mdemu, amesema ujenzi wa jengo hilo la Mahakama Kuu lilianza kujengwa mwaka 2006, na kukamilika mwaka 2015 kwa gharama ya Shilingi Bilioni 4.

 

Jaji Mkuu wa Tanzania Prof Ibrahimu Juma, wanne kutoka kushoto, akipiga picha ya pamoja na Mahakimu, mawakili mara baada ya kumaliza kuzindua Jengo la Mahakama kuu ya Kanda ya Shinyanga.

Mahakimu, Mawakili, na wadau wa mahakama wakiwe kwenye uzinduzi wa Jengo la Mahakama kuu ya Kanda ya Shinyanga.

Habari Kubwa