Majaliwa kufungua kongamano la vijana

15Aug 2019
Augusta Njoji
DODOMA
Nipashe
Majaliwa kufungua kongamano la vijana

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa leo anatarajiwa kufungua kongamano la maadhimisho ya siku ya vijana duniani ambalo litashirikisha vijana 500 nchini.

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa.

Hayo yameelezwa  na Meneja Programu na Maendeleo wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA), Dk. Majaliwa Marwa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho hayo.

Marwa amesema kongamano hilo litafanyika kwa siku mbili na kushirikisha vijana kutoka maeneo mbalimbali nchini.

Hata hivyo, amesema wakati vijana wakiadhimisha siku hiyo wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni ukosefu wa ajira.

Ametaja changoto nyingine kuwa ni ukosefu wa elimu bora na taarifa sahihi kuhusuafya ya uzazi na stadi za maisha.

Kwa upande wake, Ofisa Mawasiliano wa Shirika la Kazi Dunia (ILO)  Magnus Minja amebainisha shirika kwa mwaka huu linaadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa kwake na kwa kipindi chote masuala ya ajira ya vijana ni miongoni mwa vipaumbele vyake.

Aidha amesema Shirika hilo limekuwa linashirikiana na serikali kuweka kipaumbele cha utatuzi wa ajira kwa vijana.

Amebainisha utafiti uliofanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS) 2014 ulibaini kiwango cha ukosefu wa ajira kwa vijana ni asilimia 11.7  ukilinganisha asilimia 10.30 ya ukosefu wa ajira kwa ujumla.

Habari Kubwa