Majengo yanayovutia mji wa serikali Mtumba

25Feb 2020
Augusta Njoji
DODOMA
Nipashe
Majengo yanayovutia mji wa serikali Mtumba

Ofisi ya Rais TAMISEMI imejidhihirisha kwamba ni Ofisi ya wananchi kwa kuamua kufanya mambo magumu ambayo kwa jicho la kawaida  unaweza kusema hayawezekani. 

Jengo la Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini(Tarura), lipo katika hatua za mwisho kukamilika ikiwa ni jengo la pili la ghorofa katika mji wa Serikali Mtumba mkoani Dodoma.

Wakala huo upo chini ya Ofisi ya Rais TAMISEMI  ambayo pia imejenga ofisi yake ya ghorofa katika eneo hilo kupitia utaratibu wa 'Force Account'.

Ujenzi huo wa majengo ya Tamisemi umefanya mji huo kuvutia.

Akizungumza kuhusu ujenzi huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo, amepongeza  watu wake kwa kufanikisha ujenzi wa majengo mawili ya kisasa katika Mji wa Serikali. 

"Majengo hayo yamejengwa kwa mtindo wa Ki-TAMISEMI yaani "Force Account" ni fundisho kwa Mikoa, Wilaya, na halmashauri zote nchini juu ya umuhimu wa kujali thamani ya fedha(value for money).Hii imethihirisha usemi wa 'TAMISEMI ya wananchi'," amesema.

Habari Kubwa