Majina Matatu urais Zanzibar hadharani kesho

09Jul 2020
Augusta Njoji
DODOMA
Nipashe
Majina Matatu urais Zanzibar hadharani kesho

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa, imemaliza kikao chake na kupendekeza majina matatu ya wagombea wa urais Zanzibar kwa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC).

Hata hivyo, majina hayo yatawekwa wazi kesho Julai 10,2020 katika kikao cha NEC kwa wajumbe kwa ajili ya kupiga kura kumchagua mwanachama mmoja kwa nafasi hiyo.

Akitoa taarifa kuhusu kikao hicho leo, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole, amesema mapendekezo hayatakuwa wazi na kuwataka watu waendelee kuwa wanyenyekevu na watulivu.

“Ukifanya mchezo tu kesho tunafanya utaratibu mwingine, kwa hiyo kesho kwenye NEC tutawaambiwa wajumbe ni wakina nani kamati kuu imewapeleka NEC… wana CCM tuendelee kuwa watulivu,”amesema.

Aidha, Polepole amesema pamoja na mambo mengine kikao hicho kimetoa pongezi kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Zanzibar kwa kuimarisha uchumi wa Taifa licha ya kupitia katika kipindi kigumu cha ugonjwa wa corona.

Habari Kubwa