Maji,umeme kikwazo huduma afya uzazi Tumbatu

28Feb 2019
Rahma Suleiman
Zanzibar
Nipashe
Maji,umeme kikwazo huduma afya uzazi Tumbatu

Kukosekana kwa wataalamu wa afya,huduma ya maji safi na salama na nishati ya umeme kumekwamisha huduma za afya ya uzazi kwa akina mama kutolewa katika wodi ya wazazi ya kituo cha afya Tumbatu.

wodi ya wazazi ambayo haifanyi kazi katika kituo cha afya Tumbatu mkoa wa kaskazini unguja.

Akizungumza na Waandishi wa habari Leo Msaidizi wa kituo cha afya Tumbatu, Mcha Haji Makame amesema vifaa vyote muhimu vya huduma ya uzazi kwa akinamama kituoni hapo vipo lakini wakunga hakuna kituoni hapo.

Amesema kuwa kutokana na kuwepo kwa changamoto hiyo wananchi wa kisiwa cha Tumbatu wanajifungulia majumbani kwa wakunga wa Jadi.Alieleza kuwa kujifungulia kwa wakunga wa jadi kunaweza kukasababisha kuongezeka kwa vifo vya mama na mtoto.

Habari Kubwa