Makamba akubali kulaumiwa

09Aug 2019
Na Waandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Makamba akubali kulaumiwa

ALIYEKUWA Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira ambaye pia ni Mbunge wa Bumbuli, January Makamba amesema kama kuna pahala pamepwaya ndani ya wizara hiyo anapaswa kulaumiwa yeye.

January Makamba.

Uteuzi wa Makamba kuongoza wizara hiyo ulitenguliwa Julai 21 mwaka huu na Rais John Magufuli na nafasi yake kuchukuliwa na George Simbachawene. 

Kauli hiyo aliitoa jana Agosti 8, 2019 wakati akiwaaga wafanyakazi wa Wizara ya Muungano na Mazingira.

Katika tukio hilo alisema kuwa anawashukuru wafanyakazi hao kwa ushirikiano kipindi akiwa waziri wa wizara hiyo na kuwaomba kuonyesha ushirikiano kwa waziri mpya Simbachawene."Naomba radhi kama kuna sehemu nilikosea kwa namna moja ama nyingine," alisema Makamba na kuongeza kuwa;

"Tumefanya vitu vingi pamoja kuna mambo tumefanikiwa na kwa yale tuliyo fanikiwa ni juhudi zetu wote na kama kuna pahala tumepwaya basi lawama zije kwangu mimi," alisema

Makamba alitenguliwa nafasi yake ya Uwaziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira na Rais John Magufuli Julai 21, 2019  na nafasi yake kuchukuliwa na George Simbachawene.

Imeandikwa na Juster Prudence na Rahma Kisilwa, TUDARCO