Makonda akabidhi ofisi rasmi

03Aug 2020
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM
Nipashe
Makonda akabidhi ofisi rasmi

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda leo Agosti 03, 2020 amekabidhi Ofisi kwa mkuu mpya wa mkoa huo, Abubakar Kunenge.

Makonda ametumia nafasi hiyo kuwaaga wakazi wa Dar es salaam na kuwataka wasitie shaka kuwa ‘ataishije? Ataenda wapi?’ badala yake waumie zaidi siku wakisikia amemuacha ‘Yesu’.

Aidha Makonda amemshukuru Rais John Magufuli kwa kumuamini na kumpa nafasi kubwa, kumlinda pale alipopatwa na changamoto mbalimbali katika kipindi chote ambacho amekuwa kiongozi wa jiji hilo na kwamba yuko tayari “kumlinda Rais Magufuli hata saa tisa za usiku” wamuamshe na atasimama mstari wa mbele.

Habari Kubwa