Makonda amtaka mkandarasi wa barabara ya Biafra kujisalimisha polisi

15Apr 2019
Mary Geofrey
DAR ES SALAAM
Nipashe
Makonda amtaka mkandarasi wa barabara ya Biafra kujisalimisha polisi

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, emeendelea na ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo Wilaya Kinondoni ambapo amemtaka mkandarasi wa kampuni ya Ujenzi ya Scol Construction Ltd iliyotengeneza barabara ya Biafra chini ya kiwango kujisalimisha polisi kabla ya Ijumaa ya April 19 mwaka huu.

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo jijini Dar es salaam.

Itakumbukwa  Makonda aliagiza kampuni ya Scol na Delmont kurudia ujenzi wa barabara zilizojengwa chini ya kiwango kwa gharama zao lakini kampuni ya Delmont imekubali kurudia upya ujenzi wa barabara ya Mabatini huku kampuni ya Scol na mkandarasi wake akikaidi agizo la kurudia ujenzi wa barabara ya biafra jambo linaloleta usumbufu kwa watumiaji wa vyombo vya usafiri.

Barabara za mabatini na Biafra zilijengwa na kampuni za Scol na Delmont chini ya kiwango na kuharibika kabla ya kukabidhiwa kwa serikali jambo lililomkwaza  Makonda na kutaka zirudiwe upya kwa garama ya mkandarasi husika.

 

 

Habari Kubwa