Makonda awapa mwezi mmoja Mkurugenzi,Meya kuanza ujenzi Coco beach

09Aug 2019
Na Waandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Makonda awapa mwezi mmoja Mkurugenzi,Meya kuanza ujenzi Coco beach

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametoa mwezi mmoja kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Aron Kagurumjuli na Meya, Benjamin Sitta  kuanza ujenzi wa kuboresha ufukwe wa Coco Beach.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Agizo hilo amelitoa leo Agosti 9, 2019 baada ya kufanya ziara ya kutembelea eneo hilo na kukagua maendeleo ya mradi huo na kubaini kucheleweshwa kuanza kwa ujenzi.

"Eneo hili lilikuwa lichukuliwe na mtu binafsi lakini limerudi kwa wananchi kwa ajili ya kulifanya kuwa eneo zuri la kupumzikia watu wote," amesema Makonda na kuongeza kuwa;

“Ikumbukwe wakati Rais John Magufuli wakati ana weka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja la Coco-beach linalo unganisha Coco pamoja na Salender aliongelea mandhari ya Coco-beach na hakuishia tu kuongea Manispaa ya Kinondoni ishakuwa na "design" (mpangilio) ya namna gani ya kuboresha Coco-beach lakini kukawa na changamoto ya kesi ya hapa na pale matokeo yaliyo pelekea kutotekelezwa kwa mradi,” amesema Makonda

Ameongeza kuwa Rais Magufuli ameshatoa Sh14 bilioni kwa ajili ya kuanza ujenzi lakini hadi sasa hakuna kilichofanyika, kudai kuwa kila siku watu wanakaa vikao. “Awali kulikuwa na changamoto za kesi na kupelekea kutotekelezwa kwa mradi huu lakini zilishamalizika na fedha ipo,” amesema Makonda.

Amesema baada ya kufuatilia walielezwa kuwa mshauri ameacha mchoro ulioombewa fedha, kutengeneza mchoro mwingine wa zaidi  ya Sh40 bilioni.

"Tunatoa mwezi mmoja tutakuja kuangalia kama ujenzi umeanza,  hivyo tutarudisha fedha kwa katibu tawala na kutafuta mkandarasi mwingine,” amesema Makonda.

Imeandikwa na Kelvn Inocent na Adelina Charles, TUDARCO

 

Habari Kubwa