Malaigwanani Ngorongoro wamkataa Dk. Manongi

13Jul 2019
Zanura Mollel
Mondoli
Nipashe
Malaigwanani Ngorongoro wamkataa Dk. Manongi

VIONGOZI Wa mila jamii ya kimaasai malaigwanani zaidi ya 40 tarafa ya Ngorongoro wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha wameiomba serikali chini ya Rais Magufuli -

Alaigwanani Jamse Moringe mkazi Wa kata ya Alaitole akisoma taarifa fupi kwa Mwenyekiti Wa chama cha mapinduzi Mkoa Wa Arusha Loatha Sanare

- kubadilisha uongozi Wa mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro kutokana na kutokuwepo kwa mahusiano mazuri na jamii na kupelekea migogoro ndani ya hifadhi hiyo.

" Awali viongozi wa mamlaka waliokuwepo walikua wakikutana na malaigwanani pamoja na viongozi wa baraza la wafugaji na kujadili juu ya maisha ya wakazi na wanyama na kushauriana namana ya kuendeleza mahusiano mazuri katika hifadhi hiyo " alisema Moringe.

Akisoma taarifa fupi iliyoandaliwa na Malaigwanani hao Jamse Moringe laigwanani kutoka kata ya Alaitole mbele ya Mwenyekiti wa CCM  Mkoa wa Arusha Loatha Sanare ,amesema kutokuwepo kwa mahusiano mazuri kumeanza mwaka 2016 baada ya mabadiliko ya uongozi katika mamlaka hiyo.

" Kulikua kuna mahusianoa mazuri tangu mwaka 1992 hadi 2015 lakini kwa sasa hakuna mahusiano kati ya Wa hifadhi na wananchi" alidai Moringe. 

Katika taarifa hiyo ,malaigwanani wamelaani kuwepo kwa makatazo ya kujenga nyumba za kisasa na hata za asili kuwepo kwa makatazo ya kujenga shule ambayo ni taasisi za serikali ,kunyimwa kutumia vyombo vya moto katika maeneo ya hifadhi ikiwemo gari na pikipiki huku mazingira hayo yakiwa magumu kwa wananchi.

" Ilani ya chama cha mapinduzi inazungumzia elimu bure lakini hapa tunanyimwa kujenga shule kwa maana hiyo hakuna wawakilishi Wa Mh Rais ngazi ya wilaya hadi Mkoa ,tunataka kujua hatima yetu watu Wa tarafa ya Ngorongoro " alieleza Moringe.

"Tarafa hii ni miongoni mwa tarafa tatu zinazounda Wilaya ya Ngorongoro, ambayo ni loliondo ,sale,na tarafa hii inavijiji 25 na kata 11 pamoja na wakazi elfu 93,136 huku idadi ya Mifugo aina ya Ng'ombe ikiwa ni laki 23,800 ,mbuzi na kondoo laki 51,70 pamoja na kaya elfu 22" alisema Moringe.

Aidha alizungumzia kuwepo kwa vijana waliofukuzwa kazi kwenye mamlaka hiyo ,huku wakinyimwa ajira wazawa katika tarafa hiyo iliyopo ndani ya mamlaka na kuitaka serikali kutoka tamko rasmi juu ya vijana wasomi waliopo katika eneo hilo na wale wadarasa la saba waliofukuzwa kazi. 

Gutumuhoga kabila Mang'ati mkazi Wa kijiji cha Olpiro kata ya Easi alikemea kuwepo kwa taarifa zinazosambaa kuwa wanapewa chakula cha bure (mahindi) na huku mahindi hayo yakiwa ni ya bei nafuu.

" Tunauziwa mahindi debe moja sh 5000 na gunia moja sh 30000 alafu wanasema wanatupatia bure mahindi hayo, alidai wakazi Wa tarafa hiyo hawana imani na kiongozi Wa mamlaka hiyo ( mhifadhi mkuu Dr Fred Manongi ) " alisisitiza Gutumuhoga. 

 Fransis Siapaani kutoka kata ya Ngorongoro alisema kuwa ,kuwepo kwa manyanyaso haya ya mamlaka ya hifadhi ,kunawakumbusha mauaji ya Ndugu zao walio uwawa kinyama kwa kupigwa risasi wakiwa malishoni mwaka 1980.

" Tumeona kinachokuja kutokea sasa ndani ya hifadhi hii ni Yale yaliyotokea miaka ya nyumba ,msitukumbushe machungu,kwa nini uongozi ulivyo badilika kumeanza kwa na migongano baina ya Wa hifadhi na wananchi serikali ijitafakari" alisema Siapa.

Jamse Saringe alidai kuwa wamenyimwa kujenga nyumba za ibada ,hali ambayo wakazi Wa eneo hilo wanaishi kama wapagani ,na kumtaka mwenyekiti Wa CCM Mkoa Sanare kuruhusu ujenzi Wa nyumba za ibada katika eneo hilo.

" Inasikitisha sana tunakatazwa kujenga hadi nyumba za ibada ,inamaana serikali hii aiamini katika madhehebu ?" Alihoji Saringe

Mmoja wa wafanyakazi Toima Kipuyo mkazi wa kata ya ngorongoro waliofukuzwa kazi katika mamlaka hiyo alidai kuwa wale waliofukuzwa kazi wapo baadhi yao waliorejeshwa kazini na hii ni kutokana na undugu katika maeneo ya kazi. "

Wazawa waliofukuzwa kazi ( 61) darasa la saba kutokana na ishu ya veti, serikali ilishasema warejeshwe kazini mei mosi 2019 tuliambiwa tukitaka kurudi kazini tutoke nje ya chama cha mapinduzi CCM, tumeshindwa kujua tuelekee wapi " alidai

Naye mwenyekiti Wa CCM Mkoa Wa Arusha Loatha Sanare ambaye malaigwanani walimuita kuweza kupokea kero hizo na kumfikishia Mh Rais kwa ajili ya utatuzi alisema amepokea kero hizo na ataziwasilisha sehemu husika na majibu yataletwa kwa wakatai.

" Nimepokea malalamiko yenu malaigwanani na ni wahakikishea napeleka sehemu husika kwa majibu zaidi,nilichogundua mnawapenda wanyama lakini tatizo lililopo hakuna mahuy mazuri kati yenu na mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro " alisema Sanare