Mama matatani tuhuma za kutupa mwanawe kichakani

21May 2020
Marco Maduhu
Shinyanga
Nipashe
Mama matatani tuhuma za kutupa mwanawe kichakani

JESHI la Polisi mkoani Shinyanga linamsaka mwanamke ambaye hajafahamika jina, mkazi wa Mwakitolyo wilayani Shinyanga, kwa madai ya kumtupa mtoto wake mdogo kichakani.

Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga, Debora Magiligimba, picha mtandao

Inadaiwa kuwa alimtupa mtoto huyo mwenye umri wa miaka miwili akiwa ameviringisha Kanga.

Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga, Debora Magiligimba, alisema tukio hilo lilitokea juzi majira asubuhi, ambapo mtoto huyo aligunduliwa na wananchi akiwa ametupwa vichakani.

Alisema baada ya wananchi kumgudua mtoto huyo akiwa ametupwa vichakani, walitoa taarifa kwa Jeshi la Polisi, huku mtoto akikimbizwa kwenye Zahanati ya Mwakitolyo na kupewa huduma ya kwanza, na kwamba hali yake inaendelea vizuri chini ya uangalizi wa karibu.

“Tunamsaka mwanamke mmoja mkazi wa Mwakitolyo kwa kosa la kumtupa mtoto wake wa miaka miwili vichakani, na kumviringisha na kanga kisha kumtelekeza,” alisema Magiligimba.

Kamanda anatoa wito kwa wakazi wa eneo hilo kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi hilo ili kufanikisha mwanamke huyo akamatwe na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Habari Kubwa