Mambo waliokubaliana wakuu wa nchi Sadc haya hapa

18Aug 2019
Na Mwandishi Wetu
Dar es salaam
Nipashe
Mambo waliokubaliana wakuu wa nchi Sadc haya hapa

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Sadc), John Magufuli ambaye ni rais wa Tanzania ametaja mambo kadhaa yaliyopitishwa katika kikao cha wakuu wa nchi 16 za jumuiya hiyo kilichofanyika jana Jumamosi Agosti 17, 2019 jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Sadc), John Magufuli ambaye ni rais wa Tanzania.

Akizungumza leo Jumapili Agosti 18, 2019 kabla ya kuhitimishwa kwa kilele cha mkutano wa wakuu wa nchi hizo,  Rais Magufuli amesema wameagiza Sekretarieti kuanzisha chombo cha kukabiliana na majanga ili kuzisaidia nchi wanachama zitakapokumbwa na mafuriko, njaa na magonjwa ya milipuko.

Mkutano wa wakuu wa nchi umefanyika jana na leo na ulitanguliwa na maonyesho ya bidhaa katika wiki ya viwanda yaliyoanza Agosti 5 hadi 8, 2019 na baadaye ikafuata mikutano ya kamati ya watalaam pamoja na baraza la mawaziri wa Sadc.

"Nitoe wito kwa Sekretaieti waendelee kutumia vizuri fedha zinazotolewa na wanachama wetu na washirika wa maendeleo, hivyo basi niwaombe matumizi hayo yapelekwe kwenye miradi ya maendeleo na yasiishie kwenye semina."amesema Rais Magufuli

na kuongeza kuwa ; "Napenda kuwaomba Viongozi tushirikiane kwa kuleta maendeleo, na niwaahidi Tanzania ikiwa Mwenyekiti wa Jumuiya tutashirikiana na wanachama katika kuleta maendeleo." amesema