Mamia watoto wapata bima

17Jan 2018
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Mamia watoto wapata bima

JUMLA ya watoto 1,086 wenye umri chini ya miaka 18 ambao ni sawa na asilimia 46.2 wameandikishwa kwenye Mpango wa Toto Afya Kadi kwa ajili ya kupata matibabu kupitia mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) tangu mpango huo uanze mwaka 2016 mkoani Kilimanjaro.

Meneja wa NHIF mkoani Kilimanjaro, Fidelis Shauritanga.

Meneja wa NHIF mkoani Kilimanjaro, Fidelis Shauritanga alisema lengo la mkoa wake kwa mwaka  2017 lilikuwa ni kuandikisha watoto 3,000 lakini halikufikiwa kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo muitikio mdogo.

Changamoto nyingine, alizitaja Shauritanga, ni uelewa mdogo juu ya umuhimu wa kuwa na Bima ya Afya na baadhi ya watoto kuingizwa kwenye orodha ya wategemezi.

Alisema bado NHIF ina dhamira ya kuendelea kutoa elimu kwa jamii na kwamba wamekua wakitumia nyumba za ibada na mikutano ya hadhara katika kuelimisha juu ya umuhimu wa kuwa na bima, hususani kwa mtoto mwenye umri chini ya miaka 18.

"Kumekuwa na dhana potofu kuwa bima ya afya ni kwa ajili ya watumishi wa umma au watoto wa watumishi wa umma peke yao," alisema Shauritanga. 

 

 

Habari Kubwa