Marekani watoa msaada wa umeme Zanzibar

05Feb 2018
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM
Nipashe
Marekani watoa msaada wa umeme Zanzibar

Timu ya Maprofesa kutoka nchini Marekani imetoa msaada wa umeme jua kwa wakazi wa visiwa vya Tumbatu, visiwani Zanzibar, kisiwa ambacho kilikuwa kinakabiliwa na ukosefu wa umeme kwa muda mrefu.

Timu hiyo ya wasomi imeletwa nchini na msomi wa Kitanzania, Benjamin Fernandes, kwa lengo la kutalii pamoja na kusaidia Watanzania hasa wajasiliamali wadogo wadogo. 

 

ANGALIA ZIARA NZIMA YA MAPROFESA KUTOKA MAREKANI KATIKA KISIWA CHA TUMBATU

 Benjamin Fernandes, kijana wa kitanzania ambaye amemaliza elimu ya juu nchini Marekani katika chuo cha Stanford Graduate School of Business – MBA – California, USA 2015-2017 na kupata heshima kubwa duniani baada ya kushinda tuzo ya MBA World Summit pamoja na kubahatika kufanya kazi katika Taasisi ya Bill&Melinda Gates ya nchini humo.

MBA World Summit ni mkutano wa dunia nzima unajikita katika kuchagiza mifumo ya uongozi katika jamii, kila mwaka zaidi ya wanafunzi 100 wenye shahada ya udhamili ya biashara na uongozi kutoka katika vyuo vikuu za biashara duniani kote wanashiriki.

Habari Kubwa