Marufuku gari za mizigo kubeba abiria -Mutafungwa

14Dec 2021
Na Mwandishi Wetu
Iringa
Nipashe
Marufuku gari za mizigo kubeba abiria -Mutafungwa

MKUU wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini Wilbroad Mutafungwa, amewaagiza wakuu wa vikosi hivyo katika mikoa yote nchini kuyafanyia ukaguzi wa mara kwa mara magari ya kubeba mizigo na kwa yatakayokutwa yamepakia abiria hatua kali dhidi ya dereva husika zichukuliwe.

MKUU wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini Wilbroad Mutafungwa.

Kamanda Mutafungwa ametoa agizo hilo baada ya kukagua eneo ilipotokea ajali ya gari la kubeba magazeti, na kusababisha vifo vya watu tisa na wengine watatu kujeruhiwa katika kijiji cha Mahenge wilayani Kilolo mkoani Iringa.

Aidha, Mkuu huyo wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini amepiga marufuku magari yanayosafirishwa nje ya nchi maarufu IT kupakiza abiria kwa kuwa hayaruhusiwi kufanya hivyo.

Habari Kubwa