Marufuku kuzuia maiti kwa kisingizio gharama za matibabu

09Jun 2021
Augusta Njoji
DODOMA
Nipashe
Marufuku kuzuia maiti kwa kisingizio gharama za matibabu

SERIKALI imepiga marufuku kiongozi au mtu yeyote wa mochwari kuzuia maiti kwa kisingizio cha kutolipiwa gharama za matibabu na badala yake uwekwe utaratibu wa kulipia kadri mgonjwa anavyopata huduma ili kuondokana na changamoto ya aina hiyo pindi anapofariki.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Prof.Abel Makini.

Hayo yamesemwa leo jijini Dodoma na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Prof. Abel Makubi, wakati akizungumza na waandishi wa habari Mara baada ya kumalizika kikao cha siku tatu kilichokuwa na lengo la kujadili na kufanyia kazi maeneo ya kimkakati na maagizo ambayo yamekuwayakitolewa na viongozi wa kitaifa akiwemo waziri wa Afya, Dk.Dorothy Gwajima.

"Tayari Jana tumetoa mwongozo na barua kwenye vituo tusione Kuna mwananchi analalamika kuna maiti imezuiliwa kutoka mochwari kwa sababu yoyote ya gharama kutolipwa na badala yake uwekwe utaratibu mzuri wa kulipa gharama za mgonjwa kadri anavyopata huduma ili kuondokana na changamoto kama hii,"amesema.

Habari Kubwa