Mary Nagu akamatwa na polisi

08Mar 2018
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Mary Nagu akamatwa na polisi

Mbunge wa Hanang kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Mhe. Mary Nagu jana aliangukia mikononi mwa Polisi baada ya kukamatwa akiwa jimboni kwake katika kijiji cha Lalaj Kata ya Lalaj wilayani Hanang.

Mbunge wa Hanang kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Mhe. Mary Nagu.

Nagu alikamatwa majira ya saa 11:00 jioni kufuatia agizo la mkuu wa Wilaya ya Hanang Sara Ally Msafiri kwa madai kuwa Mbunge huyo alitofautiana maagizo na mkuu huyo wa Wilaya.

Hata hivyo Nagu aliachiwa jana hiyo hiyo baada ya uongozi wa CCM Wilaya ya Hanang kuingilia kati kutafuta suluhisho la mvutano huo ambao haujaelezwa ulikuwa unahusu nini haswa.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya Hanang Sarah Msafiri amesema aliagiza polisi wamkamate Mbunge Dkt. Mary Nagu kwa sababu alihamasisha wananchi wasishirikiane naye katika shughuli za maendeleo.