Matamasha ya utamaduni ni uchumi mkubwa - Dk. Abbasi

20Jan 2022
Na Mwandishi Wetu
Kilimanjaro
Nipashe
Matamasha ya utamaduni ni uchumi mkubwa - Dk. Abbasi

​​​​​​​KATIBU Mkuu wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Dk, Hassan Abbasi, amewataka vijana kuchukua maendeleo chanya ya utamaduni ili waweze kunufaika na kuinua uchumi wao na wa Taifa kwa ujumla.

Dk. Abbasi amesema hayo leo Januari 20, 2022 kwenye vyombo vya habari wakati alipokuwa akikagua maandalizi ya Tamasha la Utamaduni mkoani Kilimanjaro kwenye Uwanja wa Chuo cha Ushirika Moshi, ambalo litafanyika Januari 22,2022 mjini hapo ambapo Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi.

“Hivi sasa matamasha ya utamaduni katika nchi mbalimbali duniani kama lile la Reo nchini Brazil yanaingiza fedha nyingi na kuinua uchumi wa nchi zao na sisi tumeanza tunataka kutumia utamaduni kuinua uchumi wa wananchi na nchi yetu”

“Tamasha hili linakwenda kuasisi matamasha mengine lakini ndiyo njia ya kwendea kwenye tamasha kubwa kuliko yaliyowahi kufanyika nchini ambalo litajumuisha mikoa yote ambalo tumepanga lifanyike Mei mwaka huu litakalohusisha mikoa yote ya Tanzania, na litaonesha urithi wa tamaduni mbalimbali chanya tutarajie makubwa!”. Amesema Dk. Abbasi.

Aidha, amewataka vijana kuchangamkia fursa za utamaduni na kuondokana na mawazo kuwa utamaduni ni ukale na badala yake kuuenzi na kujivunia huku wakitumia utamaduni kujipatia ajira na kuboresha maisha yao.

Habari Kubwa