Akitangaza matokeo hayo visiwani Zanzibar leo Jumanne Julai 05, 2022 Kaimu Katibu wa Baraza Hilo, Athuman Amas amesema mwaka huu idadi ya ufaulu ni asilimia 99.87 ikilinganishwa na asilimia 99.62 ya mwaka jana.
"Watahiniwa 93,136, sawa na asilimia 98.97 wamefaulu. Wasichana waliofaulu ni 52, 229 sawa na asilimia 98. 55 na wavulana waliofaulu ni 52, 229 sawa na asilimia 98.55.
"Taarifa ya shule 10 za mwisho sikuionesha, nimezibainisha tu zile zilizofanya vizuri zaidi katika zile zilizofanya vizuri, kwahiyo hakuna mtu wa mwisho na ufaulu hapa ni asilimia 99.87, kwa kidato cha sita shule zote zimefanya vizuri, ila ukiwa-rank lazima atapatikana tu ambaye amewazidi wenzake kidogo, ni sawa na kusema wamepata A zote lakini mwingine ana A ya 87 na mwingine ya 89," amesema Kaimu Katibu Mtendaji