Matukio ya moto kupunguza ufaulu kwa wanafunzi 

19Jun 2019
Happy Severine
Bariadi
Nipashe
Matukio ya moto kupunguza ufaulu kwa wanafunzi 

JESHI la Zimamoto na Uokoaji nchini limesema kutokana na kuwepo wa matukio ya moto katika shule kwa mabweni kuuungua, wameamua kuanzisha programu za elimu ya kujikinga na majanga ya moto kwa wanafunzi kupitia klabu zitakazoundwa mashuleni.

aliyeshika mtungi ni mkuu wa jeshi la zimamoto moto Nchini kamishina jenerali Thobias Andengenya akitoa elimu kwa wanafunzi juu ya matumizi ya kizimamoto,pindi alipowasili shuleni hapo.

Programu hizo za elimu zitasaidia kuondoa tatizo la ufaulu kwa wanafunzi hao ,kwani wengi wao wamekuwa wakiunguliwa na vifaa vyao vya kujifunzia baada ya majanga ya moto kutokea.

Hayo yamebainishwa Leo na Kamishina Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini Thobias Andengenye alipokuwa akiongea na wanafunzi, walimu, wananchi na watumishi wa serikali mkoani Simiyu katika viwanja vya shule ya Sekondari Simiyu.

Kamishina Andengenye amesema watahakikisha majengo ya taasisi za umma na mashule yanakuwa na milango ya tahadhari  na vifaa vya kuzimia moto huku akisisitiza vifaa hivyo kutundikwa sehemu inayooneka na yenye kuweza kufikika wakati wowote.

"Ninawaomba sana watu wasidharau elimu ya kinga dhidi ya majanga ya moto...na kwa bahati mbaya watu wengi hawana elimu hiyo hivyo naomba tuungane katika kudhibiti majanga hayo" Amesema Andengenya

Katika hatua nyingine amewataka watumiaji wa majiko ya gesi kuhakikisha wanaweka mitungi hiyo nje ya nyumba ili kuepuka mlipuko ndani ya nyumba na pindi wanapoikagua wasiitikise badala yake watumie njia ya kumwagia maji.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka amesema jeshi la Zimamoto na Uokoaji liendelee kutoka hamasa ya kutoa elimu juu ya matumizi ya gesi kwa sababu watu wengi wamehamasika kutumia gesi badala ya mkaa na kuni.

Habari Kubwa