Matumizi ya mil.700/-yamshtua Waziri Ummy 

23Sep 2021
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Matumizi ya mil.700/-yamshtua Waziri Ummy 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Ummy Mwalimu amesema ataunda timu kutoka Ofisi ya Rais -TAMISEMI kuchunguza matumizi ya sh. milioni 700 zilizotakiwa kujenga bweni na bwalo katika shule ya Sekondari ya Sokoine Memorial katika Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.

Akizungumza leo wakati akikagua ujenzi wa shule hiyo, amesema  hajaridhishwa na matumizi ya fedha zilizopokelewa kwa ajili ya ujenzi wa bweni na bwalo katika shule hiyo.

"Sijaridhishwa na matumizi  ya fedha  sh. milioni 700 zilizotolewa kwa ajili ya Ujenzi wa bweni na bwalo la shule hiyo, uhalisia hauonekani" amesisitiza Waziri Ummy.

Waziri Ummy amesema kuwa wataalam hao watatakiwa kuangalia thamani ya majengo yaliyojengwa wakilinganisha na fedha zilizotumika ili kuweza kutoa ushauri  kiasi cha fedha kinachotakiwa kukamilisha  majengo hayo. 

Aidha amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuzingatia utaratibu wa matumizi ya fedha za Serikali.

Habari Kubwa