Mauaji ya kutisha, kijana aua baba, dada naye auawa

18Jan 2021
Rose Jacob
Mwanza
Nipashe
Mauaji ya kutisha, kijana aua baba, dada naye auawa

MCHUNGAJI wa kanisa wilayani Nyamagana, jijini hapa na binti yake wameuawa kikatili kwa kuchomwa kisu na mtoto wake wa kiume ambaye naye alifariki baada ya kushambuliwa na wananchi wenye hasira.

Mchungaji huyo wa Kanisa la Yesu Nakupenda Umeokoka, Beneth Karange (66) na binti yake Renatha Beneth (42), waliuawa juzi majira ya saa tisa alasiri.

Anayedaiwa kutekeleza mauaji hayo ni kijana wake wa kiume, Richmond Beneth, ambaye naye alifariki muda mfupi baada ya kufikishwa hospitali ya Sekouture, kutokana na kupigwa na wananchi wenye hasira.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Murilo Jumanne, alisema Richmond (32), alikuwa akisoma Chuo Kikuu cha Kampala kilichopo jijini Dar es Salaam.

Kamanda Muliro alisema, kijana huyo ambaye naye aliuawa, aliwachoma kisu baba na dada yake sehemu mbalimbali za mwili na kusababisha vifo vyao papo hapo.

Muliro alisema kijana huyo aliyesababisha mauaji hayo, alirudi nyumbani kutoka chuoni kwa kukosa ada.

Soma zaidi: https://epaper.ippmedia.com

Habari Kubwa