Mauzo madini Kahama yapaa

13Jan 2021
Mohab Dominick
Kahama
Nipashe
Mauzo madini Kahama yapaa

MAUZO ya dhahabu katika soko la Mwime, wilayani Kahama, yameongezeka kutoka gramu 167 kwa mwezi hadi kilo moja, imefahamika.

Hatua hiyo inatokana na Waziri wa Madini, Dotto Biteko, kufanya ziara katika soko hilo na kubaini utoshaji wa madini hayo, hivyo kuwawajibisha wahusika ikiwamo kusimamishwa kazi kwa mwenyekiti wa soko, Samuel Nalimi.

Katika ziara hiyo, watuhumiwa 11 wa utoroshaji wa dhahabu ambao ni wanunuzi, walikamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Mwenyekiti mpya wa soko hilo, Bahati Makaya, alisema juzi kwamba kwa sasa ununuzi wa madini hayo umeongezeka kutokana na hatua zilizochukuliwa pamoja na udhibiti.

Makaya ambaye ni dalali katika soko hilo, alisema tukio la kukamatwa watoroshaji hao lilitokea baada ya Waziri wa Madini kufanya ziara katika soko hilo na kubaini madudu yalikokuwa yakifanyika ikiwamo utoroshaji wa madini.

Soma zaidi: https://epaper.ippmedia.com

Habari Kubwa