Mavunde azindua kisima kata ya Chigongwe

28Feb 2021
Augusta Njoji
DODOMA
Nipashe Jumapili
Mavunde azindua kisima kata ya Chigongwe
  • Wananchi zaidi ya 10,000 kunufaika

Mbunge wa Dodoma Mjini, Anthony Mavunde amezindua kisima cha mradi wa maji ambao utawahudumia zaidi ya wananchi 10,000 wa Kata ya Chigongwe ikiwa ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa wakati wa Kampeni ya Uchaguzi Mkuu.

Mavunde aliahidi kuchimba visima 20 ndani ya mwaka mmoja tangu kuchaguliwa kwake,amewashukuru Taasisi ya Dar-Ul-Muslimeen, kwa ufadhili wa kisima hichi ambao umefikisha sasa visima 11 ambavyo vinaendelea kuchimbwa na vingine vilivyokamilika ndani ya Jimbo la Dodoma Mjini.

“Tunawashukuru sana Dar-Ul-Muslimeen kwa ufadhili wa kisima hichi cha maji,lakini pia naishukuru sana Serikali chini ya Rais Magufuli kwa kukubali kugharamia usimikwaji wa mabomba makubwa ili kusambaza maji kwa urahisi kwa wananchi wote wa hapa Chigongwe.Rai yangu kwenu ni kuwaomba wananchi kuutunza huu mradi kwa maslahi mapana ya Jamii”alisema Mavunde

Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika jana,Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Dar -Ul- Muslimeen  Muslim Bhanji amewashukuru wananchi wa Kata ya Chigongwe kwa Ushirikiano mkubwa waliouonesha wakati wa zoezi la utekelezaji wa mradi huo na kuahidi kuendelea kushirikiana na Mbunge Mavunde kutatua changamoto mbalimbali za wananchi.

Akitoa maelezo ya awali,Diwani wa Kata ya Chigongwe Simon Machelaamemshukuru Mbunge Mavunde kwa kusaidia kutatua Changamoto hiyo ya Maji ambapo awali Wananchi walikuwa wanapata tabu kupata maji safi na salama kutokana na kuwepo na maji yenye chumvi kali ambayo hayakuwa rafiki kwa matumizi ya binadamu.

Habari Kubwa