Mayweather kulipia gharama za mazishi ya George Floyd

02Jun 2020
Dotto Lameck
Nipashe
Mayweather kulipia gharama za mazishi ya George Floyd

BONDIA tajiri Duniani, Floyd Mayweather amejitolea kulipa gharama zote za mazishi ya George Floyd aliyeuawa kikatili huko Minnesota nchini Marekani kwa kukandamizwa shingoni kwa goti na Afisa wa Polisi.

Mayweather amesema kuwa, ameona umuhimu wa kushiriki katika mazishi hayo yatakayofanyika Juni 9, Mwaka huu kwa kuwa kitendo kilichotokea kwa George Floyd kimegusa ulimwengu mzima.

"Niliona ni muhimu kushiriki sababu kilichomtokea kinagusa ulimwengu mzima na sauti yake inahitajika kusikika, haswa wakati huu" amesema Mayweather.

George Floyd aliuawa wiki iliyopita kwa kukandamizwa chini kwa goti kwa zaidi ya dakika 8 na Afisa wa Polisi, Derek Chauvin.

Habari Kubwa