Mbarawa afungua mkutano bodi za mabonde, Aweso amwaga sifa

09Jul 2019
Na Mwandishi Wetu
Kigoma
Nipashe
Mbarawa afungua mkutano bodi za mabonde, Aweso amwaga sifa

Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa Leo amefungua Mkutano wa saba wa mwaka wa Bodi za Maji za Mabonde nchini pamoja na kuzindua taarifa ya faida na changamoto za ushirikiano na usimamizi wa Rasilimali za maji shirikishi pamoja na taarifa za Rasilimali maji.

Akizungumza kabla ya kuzindua mkutano huo ambao unafanyika kila mwaka, Profesa Mbarawa amesema  kama kauli mbiu ya mkutano huo inavyosema "Rasilimali za maji ni Msingi wa Maendeleo Endelevu" inakumbusha jinsi maji yalivyokuwa muhimu katika maendeleo ya nchi na watu wake.

Amesema ili kufikia uchumi wa viwanda na kufikia uchumi wa kipato cha kati unategemea kwa kiasi kikubwa kuwepo kwa rasilimali za maji katika kuanzisha, kusimamia na kuendeleza viwanda ambapo mipango mingi ya maenedeo inategemea  usalama wa maji kwa maana hiyo mkutani huo ni muhimu  kwa muktadha wa baadae.

"Kazi ya kusambaza maji kwa ajili ya matumizi ya watu na kugawa maji kwa matumizi mengine inategema sana uwepo wa maji kwa maana hiyo inawataka wizara ya maji kufanya kazi ya usimamizi kwa kushirikiana na wadau  wa rasimilai za maji kwani usipokuwepo  hakutakuwa na maji  kwa maana hiyo wadau wote wanajukumu la kulinda vyanzo vya maji," amesema Profesa Mbarwa 

Katika hatua nyingine Profesa Mbarawa amewajjia juu wakurugenzi wa Idara za maji nchini ambao wamekuwa wazembe katika usimamizi wa miradi ya maji na  kusema hatoshidwa  kuwaondoa kwenye nyadhifa zao kila baada ya miezi miwili.

"Nimewaambia pale wizarani kila mtu atakua Mkurugenzi, nitawavua nyadhifa wakurugenzi wabovu kila baada ya miezi miwili na katika suala la kugawa kazi kwa wataalam kutoka kwenye mabonde tatizo lipo kwetu  awali  wizara haikutoa fursa kwa watumishi wa mabonde kiutendaji nakiri  wizara tujikague tunapokwama mifumo  ya awali ni kupeana zabuni kwa kigezo cha asilimia 10 hata kama mzabuni ni mbovu hili sitakubali ntawaondoa,tuwatue ndoo za maji  mama zetu   "ameleza Waziri Makame.

Akifafanua changamoto ya kigoma kutopata maji ya uhakika wakati kuna mradi wenye zaidi ya Bilioni 30 Profesa Mbarawa amesema  ni kutokana na kukosa mfumo wa usambazaji wa maji ambapo, anatarajia ifikapo Agasti mwaka juu, kutenga fedha kiasi cha sh.milioni 500 kwa ajili ya uwekaji wa mfumo huo,ambao utaondoa kero ya maji manispaa ya kigoma Ujiji .

Naye Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso amefurahishwa nankazi inayofanywa na  Bodi ya Bonde la Wami/Ruvu kwa kufanya kazi nzuri ya utunzaji wa vyanzo vya maji vya bonde hilo ambalo linahudumia mkoa wa Dar es salaam, Morogoro na Dodoma.

Aweso amesema kutokana na kazi nzuri zinazifanywa na mabonde ya maji ambayo yapo tisa nchi nzima amependekeza kazi zote za utafiti katika Mamlaka za maji nchini wapewe kwani ndani ya mabonde hayo kuna wataalam wenye uwezo na weledi na kazi zao.

"Mtakapo pewa hizi kazi mfanyekazi hizo kwa kasi ili kuongeza mapato yenu na kuisaidia Wizara ya maji..Mh., nasema hivyo kwani kuna sehemu nimepita kuna watu wanafanya kazi nzuri sana.. kaka yangu Ngonyani (Afisa wa maji bonde la Wami/Ruvu) anafanya kazi nzui sana, kuna Sudi Mpemba (Afisa wa Bonde la Ruvuma) anafanya kazi nzuri sana hawa watu tuwaangalie vizuri wanafanya kazi kubwa na nzuri," amesema Aweso

Ameongeza kuwa ni lazima vyanzo vya maji vilindwe na vitunzwe kwani kuna sehemu kulikuwa na vyanzo vya maji ya kutosha lakini hivi sasa vimekauka " Lakini tunajua kabisa kuwa jukumu la kusimamia ni wazira ya maji kupitia Mamlaka za maji..Kuna Mamlaka nyingi zimekuwa hazilipi ada ya matumizi ya maji kwa kufanya hivyo watu wa mabonde wanashindwa kujiendesha," amesema Aweso

Habari Kubwa