Mbarawa ateua wakurugenzi maji

17May 2019
Na Mwandishi Wetu
DAR
Nipashe
Mbarawa ateua wakurugenzi maji

WAZIRI wa Maji, Prof. Makame Mbarawa, amefanya uteuzi wa wakurugenzi wa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira katika miji ya Kigoma, Shinyanga ma Musoma.

WAZIRI wa Maji, Prof. Makame Mbarawa.

Taarifa iliyotolewa jana ilisema Prof. Mbarawa amefaya uteuzi huo kwa mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa kifungu Na. 17 cha Sheria Na. 12 ya Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira ya mwaka 2009,

 

Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Prof. Kitila Mkumbo, ilisema katika uteuzi huo, Mhandisi Mbike Lyimo ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Kigoma (Kuwasa).

 

Kabla ya uteuzi huo, taarifa ilieleza kuwa Lyimo alikuwa Meneja wa Ufundi katika mamlaka hiyo.

 

Naye Flaviana Kifizi ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Shinyanga (Shuwasa). Kabla ya uteuzi huu, Bi Kifizi alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji na Meneja wa Rasilimali Watu na Utawala wa Shuwasha.

 

Aidha, Mhandisi Lupoja ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Musoma (Muwasa). Kabla ya uteuzi huu, Mhandisi Lupoja alikuwa akikaimu nafasi hii.

Habari Kubwa