Mbaroni kwa kumuua mama yake mzazi

10Oct 2021
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe Jumapili
Mbaroni kwa kumuua mama yake mzazi

JESHI la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linamshikilia Julius Mzava (26) Mkazi wa eneo la usalama Chang’ombe Wilaya ya Temeke kwa tuhuma za kumuua mama yake mzazi aliyefahamika kwa jina la Magdalena Peter (56) kwa kumchoma kisu sehemu ya mwili wake.

Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Jumanne Muliro.

Hayo yamethibitishwa na Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Jumanne Muliro, ambapo amesema tukio hilo limetokea Oktoba 08, 2021 majira ya saa 1:30 usiku katika eneo la Usalama Chang’ombe  wilayani Temeke wakati marehemu (mama yake) alipoiingia chumbani kwa mtoto wake Julius kwa nia ya kumpa chakula na hapo ndipo aliposhambuliwa kwa kisu eneo la mwili wake akapata majeraha makubwa yaliyopelekea kupoteza maisha licha ya jitihada za kumpeleka hospitali kufanyika.

Kamanda Muliro amesema mtuhumiwa bado anashikiliwa kwa ajili ya uchunguzi wa kina zaidi na baadaye kufikishwa mahakamani haraka.

Katika hatua nyingine Kamanda Muliro amesema kazi ya kuzui na kuwakamata waalifu wote wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu kinyume cha sharia katika Kanda Maalumu ya Dar es Salaam inaendelea katika maeneo yote.

“Kuna baadhi ya watu wanajihusisha na wizi wa magari, kuiba vifaa vya kwenye magari lakini  kuna kundi ambalo kazi yake ni kupokea vifaa vya magari, sasa hivi tumekamata watu watano, wezi wawili wanaopokea wawili na anayefuatilia wapi paibwe mmoja” amesema Kamanda Muliro.

Aidha, Kamanda huyo amesema malengo ya kanda ya Dar es Salaam ni kuhakikisha magari yote yaliyoibwa kupitia wezi hao na wapokeaji wa vifaa hivyo waliokamatwa lazima yapatikane hata kama yauzwa.

Habari Kubwa