Mbaroni tuhuma za kukutwa na vipande 10 meno ya tembo

29Nov 2020
Mary Mosha
Moshi
Nipashe Jumapili
Mbaroni tuhuma za kukutwa na vipande 10 meno ya tembo

JESHI la Polisi mkoani Kilimanjaro linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kukutwa na vipande 10 vya meno ya tembo.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Emmanuel Lukula, alisema jana kuwa watu hao walikamatwa kutokana na taarifa za siri zilizotolewa na wananchi katika Kijiji cha Kikelelwa, Tarakea wilayani Rombo.

"Tulipokea taarifa kutoka kwa raia wema, tukazifanyia kazi na kuwakamata Nicholaus Kimaro (58) na Chrispin Tarimo (56), wakiwa na vipande 10 vya meno ya tembo, yenye uzito wa kilogram 23 yakipelekwa nchi jirani," alisema.

"Jeshi la Polisi halitawafumbia macho watu wanaocheza rasilimali za taifa na tutahakikisha tunawakamata na hatua kali za kisheria zinachukuliwa dhidi yao," aliongeza.

Wakati huo huo, Kamanda Lukula alisema polisi wamewakamata watu sita wakiwa na kilo 482.78 za dawa ya kulevya aina ya mirungi na pikipiki 16.

Alisema watuhumiwa hao wengi wao ni vijana, hivyo kuwataka kuacha tabia ya kujiingiza katika vitendo hivyo.

Habari Kubwa