Mbowe ashikiliwa tuhuma za vitendo vya kigaidi

22Jul 2021
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM
Nipashe
Mbowe ashikiliwa tuhuma za vitendo vya kigaidi

Jeshi la Polisi nchini limetoa ufafanuzi kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe anashikiliwa kwa tuhuma za kula njama na kufanya vitendo vya kigaidi ikiwepo kuua viongozi wa serikali ambapo wenzeka sita walishafikishwa Mahakamani.

Akizungumza na wanahabari Msemaji wa Jeshi la polisi SACP David Misime amesema wamefikia uamuzi huo kutokana na uwepo wa upotoshaji mkubwa juu ya kukamatwa kwa mwenyekiti huyo kuwa ni kwasababu ya kupanga na kuandaa kongamano la katiba mpya mkoani Mwanza.

Amesema, jeshi la polisi halitosita kumfikisha mahakamani endapo watabaini kuna sheria aliyoivunja kutokana na uchunguzi unaoendelea kufanyika mkoani Mwanza juu ya kufanya vitendo vya uvunjifu wa amani.

Habari Kubwa