Mbowe, Matiko watinga mahakamani kwa ulinzi mkali

06Dec 2018
Hellen Mwango
DAR ES SALAAM
Nipashe
Mbowe, Matiko watinga mahakamani kwa ulinzi mkali

Ulinzi mkali umeimarishwa katika Mahakama ya Kisutu wakati msafara wa washtakiwa akiwamo Mwenyekiti Taifa Chadema Freeman Mbowe na Esther Matiko umeingia katika viunga vya Mahakama hiyo.

Msafara huo ukiwa na magari yenye ulinzi mkali wa Jeshi la Magereza na Polisi, uliingia kwa kasi huku viunga vya mahakama hiyo vikiwa na  ulinzi mkali wa jeshi la polisi walioambatana na kikosi cha mbwa wa ulinzi wa jeshi hilo.

Novemba 23,mwaka huu Mahakama ya Kisutu iliwafutia dhamana washtakiwa wawili Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko kati ya tisa wanaokabiliwa na tuhuma za kutoa lugha ya uchochezi iliyopangwa kwa ajili ya kutajwa wakati ikisubiri uamuzi wa rufani. 

Washtakiwa wengine ni, mbunge wa Iringa mjini,Peter Msigwa,  wa Kibamba,John Mnyika, wa Tarime Vijijini, John Heche, Katibu mkuu Taifa,  Vicent Mashinji,  Naibu Katibu Mkuu Zanzibar,  Salum Mwalimu,Mbunge wa Kawe, Halima Mdee na wa Bunda, Ester Bulaya.

 

Soma zaidi: https://goo.gl/fPaxfx

 

 

Habari Kubwa