Mbowe akemea vyama vya siasa kujenga ufa kwa wananchi

14Nov 2017
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Mbowe akemea vyama vya siasa kujenga ufa kwa wananchi

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe, amewaasa wananchi wa Kata ya Chanikanguo mkoani Mtwara kutoruhusu vyama vya siasa kujenga ufa miongini mwao bali viwe sehemu ya kuwapa fursa mbadala ya kupingana
kwa hoja na si uadui.

Freeman Mbowe.

Pia amewataka watu wanaohitaji mabadiliko kukipa nafasi chama hicho kwa miaka mitano na wakiona mambo wanayoyaona sasa wakihame.

Hayo amezungumza katika mkutano wa kumnadi mgombea udiwani wa Kata ya Chanikanguo, James Kaombe katika Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara jana Jumatatu Novemba 13,2017, Mbowe aliwaambia wanachama wa chama hicho na wananchi waliohudhuria mkutano huo kuwa ni ushahidi tosha kuwa Watanzania wengi wameelimika na wanataka mabadiliko ya kweli na ya kudumu.

Kwa upande wake, mgombea wa kiti hicho Kaombe amewaomba wananchi wa kata hiyo kumpa kura za ndiyo ili aweze kuunganisha juhudi zao za kujiletea maendeleo huku Mbunge wa jimbo la Ndanda Cecil Mwambwe akiwataka wananchi hao wasifanye makosa bali wamchague mgombea huyo.

Katika kampeni hizo Mheshimiwa mbowe amewapokea wanachama wapya mia tatu waliohama kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Habari Kubwa