Mbowe, Matiko washinda rufaa dhidi ya DPP

01Mar 2019
Hellen Mwango
Dar es Salaam
Nipashe
Mbowe, Matiko washinda rufaa dhidi ya DPP

Mahakama ya Rufaa imetupilia mbali rufani ya DPP ya kupinga Mahakama Kuu kusikiliza rufani ya kupinga Freeman Mbowe na Esther Matiko kufutiwa dhamana.

Mahakama ya Rufaa imeagiza jalada la kesi lirejeshwe Mahakama Kuu kwa ajili ya kuendelea kusikiliza maombi ya washtakiwa ya kutenguliwa dhamana yao.

Jopo la majaji limesema rufaa ya DPP haina mashiko na kwamba Jaji Sam Rumanyika alikuwa sahihi kukubali kusikiliza rufani ya kupinga kutenguliwa dhamana ya washtakiwa.

Mbowe na Matiko walifutiwa dhamana na aliyekuwa Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri Novemba 23v mwaka jana baada ya kushindwa kufika mahakamani kwa ajili ya kesi ya jinai inayowakabili mahakamani hapo pamoja na viongozi wengne saba wa chama hicho.

Habari Kubwa