MBOWE :Tupo katika mazungumzo na ACT-Wazalendo

03Aug 2020
Enock Charles
Dar es Salaam
Nipashe
MBOWE :Tupo katika mazungumzo na ACT-Wazalendo

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe amesema chama hicho kipo katika mazungumzo ya kufanya ushirikiano wa kuachiana nafasi ikiwemo ile ya Urais kwa upande wa Zanzibar na baadhi ya majimbo na kata nchini  na Chama cha ACT-Wazalendo.

Akizungumza katika Baraza Kuu la chama hicho, Mwenyekiti huyo amewataka wanachama wa chama hicho kuwa wavumilivu na kukubali kuachia baadhi ya majimbo watakayokubaliana kuwa watayaachia kwa chama cha ACT-Wazalendo ili kujenga mshikamano wa upinzani kuelekea uchaguzi mkuu.

“Najua wana chadema mmejenga chama chenu kwa wivu mkubwa kwa hio ukiwaambia watu lugha ya kuungana wanapata mashaka lakini tusijenge tabia ya kujimwambafai ya kwamba sisi ni wakubwa lakini tumuheshimu kila mwenzetu kwa ukubwa wake au kwa udogo wake, ukubwa wetu tujenge unyenyekevu” amesema Mbowe

Mbowe amesema kuwa  mara ya kwanza katika historia ya chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu watasimamisha wagombea katika majimbo yote  214 ya Tanzania bara na katika majimbo 50 ya Zanzibar  tayari kina wagombea  38 .

 

 

 

 

 

 

Habari Kubwa