Ziara hiyo aliyoifanya jana katika Kata ya Ukwama amekutana na wananchi kwa nyakati tofauti kuanzia kijiji cha Ihanga, Ukwama,Utweve na Masisiwe.
Akiwa katika ziara hiyo amekutana na kero ya umeme kwenye kata hizo ambapo, alisema ni jambo la kusikitisha kuona agizo la Waziri wa Nishati Kalemani alilotoa la kusambazwa umeme kwenye maeneo hayo alipofika mwaka 2018 hadi leo hakuna kinachoendelea.
"Sasa najiandaa kumfuata Waziri ili achukue hatua dhidi ya wale aliowaagiza wawashe umeme kwenye maeneo hayo...Rais ameagiza umeme ufike kila kata,kila kijiji lakini Makete leo tunazaidi ya Kata tano hazijapata umeme na vijiji vingi umeme umewashwa maeneo machache kiasi kwamba imegeuka kero kwasababu Wananchi wamesuka umeme na wameshalipia lakini wana muda mrefu hakuna kinachoendelea, Siwezi kufumbia changamoto za jimbo langu, Rais wetu ni mtetezi wa wanyonye, na sisi makete ni wanyonge kwa muda mrefu, tunaamini Rais atasikia kilio chetu na mimi nitakifikisha," alisema.
Kuhusu maji katika kijiji cha Ukwama, Sanga amewaagiza watalaamu wa Maji wafike siku ya Jumatatu wakiambatana naye wakaanze mchakato wa kutatua kero hiyo sambamba na Ihanga na Masisiwe.
Mbali na kero hizo, Sanga amechangia Mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa Bweni la shule ya sekondari na amechangia sh.500,000 kwa ajili ya kusakafia Bweni la shule ya wasichana Makete.