Mbunge aishukuru serikali Igunga kupewa mabilioni 

04Aug 2021
Na Mwandishi Wetu
IGUNGA
Nipashe
Mbunge aishukuru serikali Igunga kupewa mabilioni 

MBUNGE wa Manonga, Seif Gulamali (CCM), ameishukuru serikali kwa kuipatia Sh. bilioni sita Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, ili kutatua kero za maji.

Gulamali alitoa pongezi hizo juzi alipozungumza na Nipashe kuhusu hatua zinazochukuliwa na serikali kutatua kero za maji jimboni kwake na wilayani Igunga kwa ujumla.

Alisema ukarabati wa visima vya kienyeji kwa kuviwekea pampu mpya na kukarabati visima ambavyo pamou zake zimekufa kwa baadhi ya vijiji, kikiwamo cha Buhekela.

Alisema kazi hiyo ilianza mwishoni mwa wiki iliyopita na inaendelea kwa visima vyote vya kienyeji kwenye jimbo zima la Manonga.

Alisema mkakati huo pia unajumuisha kuangalia njia bora ya kuchimba visima au kupeleka maji ya Ziwa Victoria kwenye maeneo yote ambayo hakuna visima.

"Tunaishukuru serikali ya Mama Samia Suluhu Hassan kwa fedha walizotupatia Sh. bilioni sita kwa ajili ya kutatua shida ya maji wilayani kwetu Igunga.

"Tunasema asante sana kwa niaba ya wana Manonga," Gulamali alishukuru.

Mara tu baada ya kumalizika kwa Bunge la Bajeti Juni 30 mwaka huu, mbunge huyo alifanya ziara jimbo zima, akivifikia vijiji vyote 63 vya jimbo. 

Habari Kubwa