Mbunge ashauri kujengwa kiwanda taulo za kike

04May 2021
Augusta Njoji
Dar es Salaam
Nipashe
Mbunge ashauri kujengwa kiwanda taulo za kike

Mbunge wa Makete Festo Sanga (CCM) ameishauri Serikali kuingia ubia na sekta binafsi ili kujenga kiwanda cha kuzalisha taulo za kike.

Mbunge wa Makete Festo Sanga

Mbunge huyo ameyasema hayo wakati  akitoa mchango wake bungeni kuhusu Festo Sanga bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa mwaka 2021/22 akisema upo umuhimu wa kujenga kiwanda hicho nchini ili bidhaa hiyo ipatikane kwa wingi na kwa bei nafuu na kuwa msaada wa wanafunzi wakike.

Pia ameshauri kuanzishwa kwa wakala wa  serikali kwa ajili Vifaa vya Michezo shuleni ili kurahisisha upatikanaji wa vifaa vya Michezo shuleni ,amesema hatua hiyo itasaidia kukuza michezo nchini.

 

Habari Kubwa