Mbunge ataka uchunguzi mtambo wa kutengeneza barakoa

12May 2021
Augusta Njoji
DODOMA
Nipashe
Mbunge ataka uchunguzi mtambo wa kutengeneza barakoa

MBUNGE wa Viti Maalum, Agnesta Kaiza ameiomba serikali kufanya uchunguzi wa kina wa mtambo wa kutengeneza barakoa ulionunuliwa na Bohari ya Madawa nchini (MSD), kutokana na kutofanya kazi kwa ufanisi.

MBUNGE wa Viti Maalum, Agnesta Kaiza.

Akichangia bungeni leo hotuba ya bajeti ya Wizara ya Afya,Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa mwaka 2021/22, Kaiza amesema mtambo huo ulinunuliwa kwa dharura na kuigharimu serikali zaidi ya Sh.milioni 600 lakini unazalisha kwa kiwango cha chini.

Amesema mtambo huo ulitakiwa kuzalisha barakoa milioni nne kwa mwezi lakini hadi Septemba mwaka jana ulizalisha barakoa  320,000.

“Mpaka sasa mtambo huu umezalisha asilimia nne ya uwezo wake.Naiomba Serikali  ifanye uchunguzi wa kina kuhusiana na ununuzi wa huo mtambo wa kutengeneza barakoa wa MSD,tumenunua kwa pesa nyingi lakini cha kushangaza mtambo huo umekuwa ukizalisha chini ya kiwango," amesema.

 

Habari Kubwa