Mbunge Kapufi ahoji waliocheza mfumo wa Luku

04Jun 2021
Augusta Njoji
DODOMA
Nipashe
Mbunge Kapufi ahoji waliocheza mfumo wa Luku

Mbunge wa Mpanda Mjini (CCM), Sebastian Kapufi ametaka kujua waliokuwa wakiuchezea mfumo wa Luku na kusababisha watu kukosa huduma hiyo walikuwa wanapeleka ujumbe gani kwa Taifa.

Mbunge wa Mpanda Mjini (CCM), Sebastian Kapufi.

Mbunge huyu amehoji suala hilo jana Alhamisi Juni 3, 2021 wakati akichangia bajeti ya Wizara ya Nishati kwa mwaka 2021/22. 

Kapufi amesema mfumo huo umewezesha mapato ya Shirika la Umeme nchini (TANESCO)  kuongezeka kutoka Sh.Bilioni 72 mwaka 2016 hadi kufikia Sh. Bilioni 160 mwaka 2020/21.

Kuhusu sekta ya gesi nchini, Kapufi ameshauri Serikali iendelee kufanyia rejea kwenye taarifa iliyotokana na kamati maalum ya Bunge iliyoundwa na Ndugai ya kumshauri kuhusu sekta hiyo. 

Habari Kubwa