Mbunge Chadema aigaragaza serikali mahakamani

10Aug 2018
Nebart Msokwa
MBEYA
Nipashe
Mbunge Chadema aigaragaza serikali mahakamani

Mbunge wa Jimbo la Mbozi mkoani Songwe, Pascal Haonga (Chadema) na wenzake wawili wameachiwa huru na Mahakama ya Wilaya ya Mbozi baada ya kuigaragara Jamhuri kwenye kesi ya jinai iliyokuwa inawakabili mahakamani hapo.

Pascal Haonga

Haonga na wenzake, Mashaka Mwampashi pamoja na Wilfredy Mwalusanya walikuwa wanakabiliwa na kesi ya jinai wakidaiwa kufanya vurugu na kuharibu uchaguzi wa Mwenyekiti wa Mji wa Mlowo uliofanyika Agost 28, 2017.

Watatu hao ambao wote ni wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) walikuwa wanakabiliwa na makosa matatu waliodaiwa kuyatenda Agosti 28, 2017.

Katibu Mkuu Chadema Dk Vicent Mashinji, mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Nyasa, Mchungaji Peter Msigwa na katibu wake, Emmanuel Masonga walikuwepo katika mahakama hiyo kusikiliza hukumu ya Mbunge Haonga na wenzake.

Akisoma huku hiyo leo hakimu mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Nemes Chami amesema katika mashtaka yote matatu, upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha makosa.

"Katika ushihidi wa mashahidi sita wa upande wa Jamhuri hakuna mahali walipothibitisha kwamba washtakiwa walikataa kukamatwa,” amesema.

“Hakuna mahali walipoonesha kwamba washtakiwa hawa waliwazuia askari kutekeleza majukumu yao na hakuna mahali walipothibitisha kwamba washtakiwa walilazimisha kurudi ukumbini baada ya kutolewa nje.”

Amesema kutokana na upande wa Jamhuri kushindwa kuthibitisha ushahidi wa mashtaka waliyoyawasilisha mahakamani hapo, mahakama inawaachiria huru washtakiwa wote.

Soma: https://www.ippmedia.com/sw/habari/mbunge-chadema-aigomea-polisi

Habari Kubwa