Wilaya hiyo inakabiliwa na wimbi kubwa la mbwa wanaozurura na hawana chanjo jambo ambalo lisipochukuliwa hatua za haraka linaweza kusababisha madhara kwa jamii.
Wajumbe wa Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo, wamekubaliana kufanya operesheni ya kuwauwa mbwa wote wanaozurura.
“Mbwa wamekuwa wengi sana mitaani kwetu, ukiingia mtaani kitu cha kwa kwanza kukutana na mbwa wakizurura ovyo na suluhisho lake ni kuwauwa kwa kuwapiga risasi, Tulikuwa tunakabiliwa na ukosefu wa risasi, lakini tayari risasi zimepatikana na kinachofuata ni kuanza zoezi mapema,” alisema Diwani wa Kata ya Karansi, Dancan Urasa.
Naye Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Frank Tarimo, amesema ili kukabiliana na tatizo hilo, halmashauri kupitia idara husika wataanza kuwaua mbwa wote watakaokutwa wanazurura na tayari vitendea kazi vimeshaandaliwa.