Meneja Bandari mbaroni tuhuma kupokea rushwa

03Jul 2020
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Meneja Bandari mbaroni tuhuma kupokea rushwa

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), imemkatama aliyekuwa Meneja wa Bandari ya Kipumbwi, Steven Mbakweni, kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa.

Na Fatma Mtutuma, UDOM

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kaimu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa Tanga, Anthony Gang’olo, alisema Mbakweni aliomba rushwa ya Sh. 900,000 kwa mteja wake kwa ajili ya kumruhusu asafirishe mzigo kutoka Pangani kwenda Zanzibar.

“Uchunguzi wa TAKUKURU ulibaini kwamba Mbakweni aliomba na alishawishi hongo baada ya mteja wake kumpatia nyaraka zote zilizotolewa na ofisi ya Bandari baada ya kufanya malipo ili kusafirisha mzigo wake katika bandari hiyo,” alifafanua Gang’olo.

Aliongeza kuwa: “Nyaraka hizo zilikataliwa na Mbakweni kwa madai kwamba hazitambui akiwa na lengo la kushawishi apewe hongo ya Sh. 900,000 kwa ajili ya kusafirisha mzigo huo.”

Gang’olo alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa baada ya kupokea rushwa ya Sh. 270,000 kama mtego baada ya mteja huyo kuomba apunguziwe.

“Mtuhumiwa alikamatwa katika bandari ya Kipumbwi majira ya saa 9:00 alasiri akiwa amepokea rushwa ya Sh. 270,000 baada ya mteja kubembeleza apunguziwe,”alisema Gang’olo.

Mkuu huyo alitoa onyo kwa watumishi wa umma wenye tabia hizi hususani katika kipindi hiki cha uchaguzi kuwa kitendo hiko ni kosa chini ya kifungu cha 15 cha kupambna na kuzuia rushwa.

Habari Kubwa