Mfanyabiashara atoweka Dar

07Dec 2018
Adam Fungamwango
DAR ES SALAAM
Nipashe
Mfanyabiashara atoweka Dar

MFANYABIASHARA Nasser Islam (48), hajulikani alipo kwa muda wa miezi tisa sasa, baada ya kuondoka nyumbani kwake akiaga kuwa anakwenda Chato kwa ajili ya biashara.

MFANYABIASHARA Nasser Islam.

Kwa mujibu wa mke wake Sabaha Awadhi, Nasser aliondoka nyumbani kwake Kariakoo jijini Dar es Salaam Machi 9, mwaka huu, akiaga kuwa anakwenda Chato kwa ajili ya biashara zake, lakini mpaka sasa hajarejea na wala hapatikani kwenye njia zake zote za mawasiliano.

“Tumehangaika kote ambako tunadhani kuwa tungempata, lakini hatujafanikiwa, vituo vya polisi na hospitali zote tumemaliza,” alisema Sabaha.

Mke wa mfanyabiashara huyo alisema kuwa, baada ya kushindikana kote waliamua kutoa ripoti kwenye Kituo cha Polisi Geita na kupata hati ya taarifa namba RB/GE/2731/2018.

Aliomba yeyote atakaye bahatika kumuona au kupata taarifa zake atoe taarifa kwenye kituo cha polisi kilicho karibu naye au kupiga simu 0713 988611 au 0718 282888.

Habari Kubwa