Mfumo mpya ukusanyaji mapato TARURA watambulishwa

20Jul 2021
Neema Emmanuel
MWANZA
Nipashe
Mfumo mpya ukusanyaji mapato TARURA watambulishwa

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel leo ametambulisha mfumo mpya ulioboreshwa wa ukusanyaji wa mapato kwa njia ya kielektroniki ujulikanao TeRMIS uliopo chini ya wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA).

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel.

Amesema ukusanyaji wa mapato yatokanayo na maegesho ya vyombo vya moto na hifadhi za barabara malipo yake yote yatafanyika kwa kutumia mfumo huo wa kielektroniki kwa kutumia kumbukumbu namba ya malipo ambayo yatapokelewa moja kwa moja serikalini.

Ameongeza kuwa mfumo huo utaongeza ufanisi wa ukusanyaji mapato yatakayosaidia maboresho na maendeleo ya miundombinu ya barabara, kusaidia wateja kufanya maombi na kulipia huduma kwa njia ya mtandao bila kufikia ofisi za TARURA.

" Natoa wito kwa wananchi wote kupokea mabadiliko haya yalioanza kutekelezwa leo na kuhakikisha wanalipa wenyewe ushuru wa maegesho ili kuepuka adhabu na faini zisizo na lazima pia elimu itaendelea kutolewa mfumo huu utafanya vizuri kwani maboresho haya ni ya kimageuzi"  amesema 

Kwa upande wake Mhandisi Shadrack Mahenge Afisa TEHAMA wa TARURA ameeleza kuwa mfumo huo ulianza kutumika Mwanza Julai 20 mwaka huu unampa fursa mteja kulipia ushuru wa maegesho kwa saa,masaa,siku,wiki au mwezi.

Habari Kubwa