Mfumuko wa bei wapaa kwa Novemba

10Dec 2019
Augusta Njoji
Dodoma
Nipashe
Mfumuko wa bei wapaa kwa Novemba

MFUMUKO wa bei kwa mwaka unaoishia mwezi Novemba 2019, umeongezeka na kufikia asilimia 3.8 kutoka asilimia 3.6 ya mwezi Oktoba.

Kaimu Mkurugenzi wa sensa ya watu na takwimu za jamii, Ruth Minja, picha mtandao

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Kaimu Mkurugenzi wa sensa ya watu na takwimu za jamii, Ruth Minja, amesema bei zimeongezeka kutokana na mahitaji ya bidhaa sokoni kuwa makubwa.

Aidha, bidhaa za vyakula na visivyo vya vyakula vimechangia kuongezeka kwa mfumuko huo.

Minja amesema bidhaa hizo ni pamoja na mchele, nyama, unga wa muhogo, mihogo, mafuta ya kupikia, mboga mboga, maharage, mavazi, mkaa, thamani, mazulia na huduma ya malazi ya nyumba za wageni.

"Mahitaji ndio yamesababisha kupanda kwa bei za bidhaa hizi na inawezekana inachangiwa na uhaba wa uzalishaji na usafirishaji," amesema Minja.

Habari Kubwa