Mgodi wa GGM kufikishwa mahakani

02Aug 2017
Frank Monyo
Nipashe
Mgodi wa GGM kufikishwa mahakani

Halmashauri ya mji wa Geita imeipa mwezi mmoja kampuni ya madini ya dhahabu ya Geita (GGM) kulipa dola za Marekani milioni 11.045 ambazo ni madai ya ukwepaji wa tozo ya huduma kwa kipindi cha mwaka 2004 hadi 2013 na endapo utashindwa, utapelekwa Mahakamani.

Mgodi wa GGM ulianza uzalishaji mwaka 2000 na kuingia makubaliano na Wizara ya Nishati na Madini ya kulipa dola 200,000 kwa halmashauri kila mwaka, lakini inadaiwa haikulipa tangu 2004 kwa madai kuwa halmashauri haina sheria inayoelekeza walipwe kiasi hicho.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Geita, Leonard Bugomola amesema kuwa wametoa siku 30 fedha zilipwe na endapo hawatalipwa, wataupeleka mgodi mahakamani kwa kuwa sheria zipo wazi.

Habari Kubwa