Mgombea Urais ADC aahidi ajira milioni 10

19Sep 2020
Boniface Gideon
Tanga
Nipashe
Mgombea Urais ADC aahidi ajira milioni 10

Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha ADC Queen Cuthbert Sendiga amesema endapo atapata ridhaa ya Watanzania ya kuwa Rais atahakikisha anatengeneza ajira zaidi ya milion 10 kwakipindi Cha miaka mitano 2020/2025 ili kuondoa changamoto ya Ajira iliyopo hivi sasa nchini.

Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha ADC Queen Cuthbert Sendiga:PICHA NA BONIFACE GIDEON

Akizungumza  Leo  septemba  19 na Wananchi wa wilaya za Mkinga (Maramba)  na Korogwe ( mashewa) wakati wa mikutano ya Kampeni  za Uchaguzi  Mkuu  ,Mgombea huyo wa Urais alisema atahakikisha anatengeneza miundombinu ya barabara ,kilimo , elimu na afya ili kurahisisha huduma za kijamii hali ambayo italifanya Taifa kuongeza kiwango cha ajira nchini.

Aliongeza kuwa atahakikisha anakuza sekta ya uvuvi  pamoja na kujenga  viwanda  vya usindikaji wa mazao hivyo ndani ya miaka mitano ijayo ambapo zaidi ya ajira milion 10 zitatengenezwa 

" Naomba  ikifika Oktoba 28 mnipigie kura niwe Rais wenu ili niweze kutekeleza haya yote , wavuvi mtanufaika na ajira yenu ambapo nitawajengea viwanda vyakusindika  samaki na mtauza kwa bei nzuri nakuondokana na adha ya uhaba wa masoko" amesema Sendiga.

Habari Kubwa